calvinpaul131@yahoo.com

Friday, September 20, 2013


LUCCI AMVALISHA PETE MCHUMBA WAKE - JOKETI ABAKI KUWA KAKA NA DADA

lucci2 
PRODUCER WA HIT NYINGI MJINI LUCI
lucci 
Hivi sasa producer wa wimbo wa kaka dada ameamua kumvisha pete mpenzi wake ambaye amekuwa mchumba wake rasmi.Cheki picha hapa na Lucci akiongea na millardayo.com alisema,
“Baada ya mambo project ya Kaka Dada kukamilika nimeona ni muda muafaka kabisa kumvisha pete mpenzi wangu Lisa Semgeliwa au marafiki zake huwa wanamuita Lizzyblazzer. Unajua like seriously tumekuwa kwenye dating kwa muda zaidi ya miaka 2. Muda huo unatosha kabisa naamini ni vizuri kuingia kwenye hatua nyingine ya mahusiano yetu” .

SERENGETI FIESTA MOROGORO ILIKUA HIVI JANA USIKU

Chezea Shilole wewe
SHILOLE KAZINI NA SHABIKI YAKE WAKIMALIZA  STEJINI
Chege na kundi zima la wanaume family.
CHEGE CHIGUNDA NA MH . TEMBA TOKA TMK WANAUME
Wana wa Chamber Squad
CHEMBER SQUAD WALIMALIZA SHUGHULI HAPA
Nay wa Mitege akicheza kwa style yake mpya,
DIAMOND NA NAY WA MITEGO WAKISHAMBULIA JUKWAA

ZAIID - WHO DAT - KANDA MBOVU MIX TAPE HII HAPA VIDEO

Saturday, April 6, 2013

Ban Ki Moon aisihi N Korea kutuliza joto

 5 Aprili, 2013 - Saa 06:56 GMT
Korea ya Kaskazini yazidisha nguvu za kijeshi
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki moon ameitaka Korea ya kaskazini kupunguza makali yake kwa mzozo unaotokkota wa kinuklia akisema kuwa umeanza kuvuka mpaka.
Bwana Ban amesema kuwa anahuzunishwa na namna ugomvi huo unavyotishia maisha ya wananchi wa kawaida.
Akizungumzia vitisho vya karibuni sana vya Korea Kaskazini kwa Korea Kusini na Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon alisema kuwa hali hiyo imekuwa ya kustajabisha na kusikitisha.
Alisema kuwa Korea Kaskazini imezidisha vitisho vyake na akaonya kuwa cho chote kinaweza kuzusha kitendo cha kusikitisha.
Bwana Ban aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Umoja wa Mataifa, alitoa wito kwa viongozi wa Korea kaskazini kubadili mwenendo wao.
silaha kali
Awali msemaji wa Wizara ya mashauri ya Kigeni wa Urusi alisema kuwa uamuzi wa Korea Kaskazini kuendeleza mpango wake wa kuimarisha uwezo wake wa zana za kinukilia unavuruga mipango ya kuanzisha upya mashauriano yanayohusu mataifa sita ya kupatanisha Korea Kusini na Kaskazini.
Mataifa yanayokusudiwa kushiriki katika mashauriano hayo ni Korea Kusini, Korea Kaskazini, Uchina, Urusi, Japan na Marekani.
Msemaji huyo alieleza kwamba juhudi zo zote za kupuuza maazimio ya Umoja wa Mataifa hazikubaliki.

Saturday, November 10, 2012