Ban Ki Moon aisihi N Korea kutuliza joto
5 Aprili, 2013 - Saa 06:56 GMT
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa
Ban Ki moon ameitaka Korea ya kaskazini kupunguza makali yake kwa mzozo
unaotokkota wa kinuklia akisema kuwa umeanza kuvuka mpaka.
Bwana Ban amesema kuwa anahuzunishwa na namna ugomvi huo unavyotishia maisha ya wananchi wa kawaida.Akizungumzia vitisho vya karibuni sana vya Korea Kaskazini kwa Korea Kusini na Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon alisema kuwa hali hiyo imekuwa ya kustajabisha na kusikitisha.
Alisema kuwa Korea Kaskazini imezidisha vitisho vyake na akaonya kuwa cho chote kinaweza kuzusha kitendo cha kusikitisha.
Bwana Ban aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Umoja wa Mataifa, alitoa wito kwa viongozi wa Korea kaskazini kubadili mwenendo wao.
Mataifa yanayokusudiwa kushiriki katika mashauriano hayo ni Korea Kusini, Korea Kaskazini, Uchina, Urusi, Japan na Marekani.
Msemaji huyo alieleza kwamba juhudi zo zote za kupuuza maazimio ya Umoja wa Mataifa hazikubaliki.
Rais Mpya wa CAR akataliwa na viongozi
Rais mpya wa Jamhuri ya Afrika
ya Kati amesema kuwa amekubali matokeo ya mkutano wa dharura wa viongozi
wa eneo hilo ambao wameafikiana kutotambua rasmi uongozi wake.
Mkutano huo uliofanyika nchini Chad ulimtaka
bwana Mitchel Djotodia aunde baraza la mpito kusimamia nchi hiyo na
kuandaa uchgauzi katika miezi kumi na nane ijayo.Awali wanajeshi wake waasi walipotwaa uongozi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, na kumfukuza aliyekuwa rais Francois Bozize, bwana Djotodia alisema kuwa hata achia mamlaka hadi atawale miaka mitatu.
Wakati huo huo, nchi Jirani ya Chad imekanusha madai yaliyotolewa na rais aliyeondolewa mamlakani Francoise Bozize, kwamba nchi hiyo iliwasaidia waasi kupindua serikali yake.
Waasi wa Seleka walivamia mji mkuu Bangui na hatimaye kumfurusha rais Francoise Bezize kutoka kasri lake mwezi mmoja uliopita.
No comments:
Post a Comment