calvinpaul131@yahoo.com

Saturday, October 20, 2012


Friday, October 19, 2012

FROLAH MVUNGI ATOLEWA MAHARI NA KUVISHWA PETE NA H - BABA LEO

 
 
 Tukio la kihistoria linafanyika jumamosi ya leo katika hotel ya atriums pale  ambapo wasanii wawili kati ya FROLAH MVUNGI NA HAMIS RAMADHANI H-BABA watakapovishana  pete ya uchumba na utoaji wa mahari hapo hapo. Tafrija hii fupi itaanza saa 10 jioni nakumalizika baada ya masaa mawili baadae. Akiongea na xdeejayz flora alisema leo ni siku yake yafuraha sana anatamani muda ufike hili tukio hili lifanyike kwa aman na kidole chake kiwe na pete ya uchumba. XDEEJAYZ INAWATAKIA SHEREHE NJEMA.

 FROLAH MVUNGI

HAMIS RAMADHANI H-BABA

DALASS(wa wolper) AMPORA BOB JUNIOR GARI

 

Taarifa zilizopo town kwa sasa ni kitendo cha mkurungenzi wa dallas enertainment dallas(roho ya wolper) kumnyang'anya gari aliyokuwa akitembelea bob junior,kwa madai ni ya kwake na alimpa atumie tu!nilimtafuta bob junior na mkasa ulikua hivi "

DALLAS NI KAMA BOSS WANGU LAKINI PIA NI NDUGU YANGU UPANDE WA MAMA NA NDIO UKARIBU WA BIASHARA ZOTE NINAZOFANYA NAE,KUHUSU GARI KWELI ILIKUA MALI YAKE LAKINI ALIKWAMA KUNA KIPINDI WAKATI YUPO EUROPE AKANIAZIMA PESA NA AKANIPA GARI aina ya GX 110,KAMA DHAMANA,NA ALIENDELEA KUCHUKUA PESA MPK IKAFIKA ML KAMA 9 AU 8 NIKAWASILIANA NAE KUHUSU KUNIUZIA GARI ILI NIMALIZIE KILICHOBAKI ILA HAKUA TAYARI KUPOKEA PESA ILA ALINIAMBIA PESA ILIYOBAKI NI MCHANGO WA KUNISAPOTI KUPATA GARI MPYA,SO JUZI NMESHANGAA ANAKUJA ANASEMA NIMMALIZIE PESA YA GARI ANASHIDA SIKUWA TAYARI KUMPA HIYO PESA SO NIKAMWAMBIA ATAFUTE MTU AMUUZIE THEN ANIPE PESA YANGU ACHUKUE PESA YAKE ITAKAYOBAKI BAADA YA KUTOA ML.8 YANGU JUZI NIMEKUTANA NAE AMECHUKUA GARI MPK LEO HAJARUDISHA SO SIELEWI KAMA KALIUZA AU VIPI ILA KADI NIPO NAYO MIMI NA SIWEZI KUITOA MPAKA ANIKABIDHI PESA YANGU"


PICHA CHINI NI STUDIO KWA BOB JUNIOR AKIWA NA KADI YA GARI ALILOTAPELIWA NA DALLAS


BOB junior akinionesha kadi ya gari hiyo!



BOB JUNIOR

WANANCHI WAINGIA KWENYE MAGARI BILA YA KUJUA WANAPOELEKEA KWA KUOGOPA MABOMU YA MACHOZI

TISHIO LA MAANDAMANO LILIVYO ATHIRI USAFIRI KWA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM "PICHANI" WANANCHI WAKIGOMBEA KUPANDA DALADALA MAENEO YA POSTA JIJINI!
Mitaa ya Uhuru kama unavyoonekana ikiwa haina watu wa kutosha kutokana na wasiwasi wa vurugu za maandamano ya Waislamu.Huku muda mwingi magari ya Jeshi la Polisi yalionekana kuranda randa kwenye viunga vya mitaa hiyo ikiwa ni tahadhari ya kuthibiti uvunjifu wa amani.Ambao ungeweza kutokea
TUMEDHIBITI MAANDAMANO:KAMANDA KOVA
Wengi watiwa mbaroni!
Jeshi la Polisi Kanda Maalum  Dar Es Salaam limesema kuwa limeweza kudhibi maandamano ya Waislamu yaliyokuwa yafanyike Ijumaa ya leo kushinikiza kuachiwa huru kwa wenzao wanaoshikiriwa na Jeshi hilo kwa tuhuma mbalimbali za uvunjifu wa amani.

Akionge na waandishi wa blog hii Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam Bw. Suleiman Kova alisema” Jeshi letu limefanya kazi kubwa na nzuri kwa kuzuia maandamano hayo ambayo yangeweza kuleta uvunjifu wa amani kwa wananchi wasio kuwa na hatia” Alisema Kamanda Kova

Aidha Kamanda Kova aliongeza kusema kuwa watu kadhaa wanashikiriwa na Jeshi hilo kwa kukiuka agizo la Serikali kupitia Jeshi hilo.Hata hivyo timu wanahabari wetu waliokuwa mitaani kwa ajili ya kukusanya matukio walishuhudia katikati ya mji maduka yakiwa yamefungwa na hakuna kilichokuwa kinaendelea.

Mmoja wa wanafabiashara wa mitumba maeneo ya Mtaa wa Kongo alisema kuwa” Jamani tuliamua kusimama baishara zetu kwa kuhofia usalama wetu na mali lakini tunashukuru Mungu amesaidia hivyo hivyo” Alisema kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Ibarahim.

Thursday, October 18, 2012

MAGDALENA ROY AWA TOP MODEL REDDS MISS TANZANIA 2012

 Mshindi wa Top Model Redd's Miss Tanzania 2012, Magdalena Roy katika shindano lililomalizika kwenye ukumbi wa hoteli ya Naura Springs, Jijini Arusha

 MAGDALENA KATIKA POZI

MISS ILALA ALICHUKUA NAMBA MBILI NA MISS DAR CITY CENTER PIA ALICHUKUA NAMBA MBILI MISS TANZANIA JE?

Wednesday, October 17, 2012

ANTI BILALI KWENYE KITCHEN PARTY NA SINTA

 Hule utamaduni wa sherehe za kitchen party, unaohudhuliwa  na wakina mama peke yake kama unaanza kupotea siku hizi baada ya sherehe hizo kuingiliwa na wanaume ambao wanasemekana ni mashoga kwa kiasi kikubwa sana.mashoga hao ujichanganya na kina mama kama na wao ni wanawake na wengine mpaka kuingia katika vyoo vya kike na wakiwa wanajisaidia haja ndogo  uchuchumaa kama wakina mama.

 Sinta na ant bilali

 Anti  bilali akimtunza mwali

Anti bilali na kipochi chake akiwa na shoga zake

The Secret of Life: Happy and Successful

The secret of life is going to be different for us all, as we all have different goals and ideals we set for ourselves and want to achieve. However, I think that some universal secrets to a happy and successful life are:-
To think outside of yourself so that you are adding to the world rather than just taking away. By finding ways to help others to get what they want we are able to help ourselves without trying.
When we help others we are in the right place and we do not struggle so much. This means we worry less and spend more time thinking positively and less time sulking around wining about what we don’t have, or what we haven’t yet got round to doing.
Lend a helping hand to those people who seek help. People who suffer emotional pain/ problems; you can cheer them up by giving them motivational words. Letting them know that they are not alone and that there is no problem without a solution.
Being there when someone needs you brings joy to your heart. Though you can’t necessarily help that person directly, the essence that you’re there willing to listen and comfort her/him is really a big help to them. Helping someone by heart brings true joy, and that person will never forget you, and will always be there when the time comes that you’re the one who needs help. So it’s good helping other people without asking in return.
As they say, ‘life is what you make it’. Plus it’s pretty short so make the best of it. You’re not here very long at all! If you live your life in misery then the secret of  life sucks, but if you try to spend every waking moment enjoying life, then you realize that life is a privilege, so take advantage.
Therefore by helping others we are automatically helping ourselves. So I spend a fair bit of my time just looking for ways to help those around me. Then as if by magic more good things happen to me. And what’s more they often come to me from completely un-associated areas.
Share and Enjoy:
  • Ping.fm
  • Yahoo! Buzz
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • Blogplay
Tags: , ,
This entry was posted on Saturday, April 17th, 2010 at 2:06 pm and is filed under DNA The Secret Of Life, Is The Secret Of Life, Secret Lives Of Famous People, Secrets Of Life, The Secret Of Life
























Monday, October 8, 2012













GROW Ambassedor

GROW Ambassedor

06/01/2011 Kanumba, GROW Ambassedor
MSC

MSC

07/19/2011 KANUMBA at Mama Shujaa Wa Chakula
HOLLYWOOD (Los Angeles)

HOLLYWOOD (Los Angeles)

04/08/2011 Kanumba In HOLLYWOOD
New York City

New York City

04/08/2011 Kanumba In New York City (NYC)
Kanumba The Great & Ramsey

Kanumba The Great & Ramsey

04/18/2011 Kanumba The Great & Ramsey Nouah (From Nigeria) In Tanzania
VOA

VOA

04/08/2011 Kanumba In VOA(Voice Of America)
FilamuCentral

FilamuCentral

04/08/2011 Kanumba In FilamuCentral Awards
Zanzibar

Zanzibar

04/08/2011 Kanumba in Jan'gombe Sec. School
Congo

Congo

04/08/2011 BujumburaKanumba In Congo

Bujumbura

04/08/2011 Kanumba In Bujumbura












Friday, October 5, 2012





Ronaldo after being amazed by his own goal in Real Madrid's win over Deportivo La Coruna on Sept. 30.
Wednesday, October 3, 2012 12:59 PM


Ufisadi Chunya unatishia ustawi wa wafugaji

June 3rd, 2012 | by Albano Midelo
“MAISHA yetu ni kama kifaranga aliyekosa mama kwani hali zetu za kiuchumi kila kukicha zinazidi kudhoofika kama mgonjwa wa kwashiakoo’’,anasema Julius Machia  ambaye ni kiongozi wa kikundi cha umoja wa wafugaji wahamiaji bonde la Songwe lililopo wilayani Chunya mkoani Mbeya.
Anabainisha kuwa endapo kiwango cha kupigwa faini ambazo sio halali  kitaendelea ,mifugo yao itamalizika  na watakuwa masikini na mzigo kwa  serikali  kwa  kuwa wanaishi kwa kutegemea mifugo walionayo.
Machia anasema tangu zoezi la kukamata mifugo inayozidi 70 na kutozwa kwa kila mfugo unaozidi shilingi 20,000,kumesababisha matatizo mengi kwa wafugaji yakiwemo baadhi yao kuuwawa na askari kwa kupigwa risasi katika operesheni ya kamata mifugo na wafugaji kudhulumiwa kwa kupigwa faini kubwa hali ambayo inamlazimu mfugaji kuuza mifugo kwa bei ya hasara.

Hii ni risiti ambayo amepewa mfugaji baada ya kupigwa faini ya uharibifu wa mazingira ,hata hivyo mfugaji alitoa shilingi milioni sita ikiwa ni faini ya ng’ombe 300 sawa na kila mmoja shilingi 20,000,hata hivyo mtendaji ameandika shilingi  600,000 tu
“Kwa miaka 10 sasa zoezi la kukamata mifugo, limekuwa  kama mvuta sigara huvuta  sigara anapojisikia kiu kwa kuwa watendaji wa serikali wanaendesha zoezi hili bila mpangilio na limekuwa linafanyika mara kwa mara tena kwa unyanyasaji mkubwa’’,anasisitiza Machia. Julius Machia anasema faini wanayotozwa na serikali kwa kila mfugo unaozidi  imekuwa inafanyika katika mazingira ya kifisadi kwa kuwa kiwango cha faini ni kikubwa na kwamba kinachoandikwa kwenye risiti za malipo ya Halmashauri ya wilaya na hali halisi ni tofauti.

Ngombe wa wafugaji wahamiaji wakisubiri kuuzwa kwa bei ya hasara mnadani ili kuweza kulipa faini ambazo wanatozwa na Halmashauri zikiwemo mazingira, kulisha mashamba na faini nyingine.
Baadhi ya risiti ambazo gazeti hili imepata nakala zake zinaonesha kuwa  mfugaji Materemki Lugola wa kijiji cha Wanzani alilipa faini ya shilingi milioni 4,740,000 mwaka 2001 kwa ajili ya mifugo 948 kula katika mashamba ya wakulima.
Aliyetakiwa kupokea fedha hizo  ni mkulima ambaye shamba lake limeliwa na mifugo kupitia ofisi za vijiji badala yake mpokeaji wa fedha hizo ni Afisa mifugo,kilimo na ushirika wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ambaye amesaini katika risiti kuwa amepokea kiasi hicho cha fedha.
Risiti nyingine ya mwezi Mei mwaka 2011 inaonesha kuwa mfugaji Julius Machia wa kijiji cha Chang’ombe  alilipa faini ya shilingi milioni sita kwa ajili ya kuzidi mifugo 300 ambapo kila mfugo uliozidi ulitozwa shilingi 20,000,hata hivyo risiti hiyo imeandikwa mfugaji huyo amelipa shilingi laki sita badala ya milioni sita.
“Tumepumzika kwa miezi sita,tu Mei 16 na Juni mosi mwaka huu afisa mifugo akiwa na viongozi wengine wamefika tena kwenye bonde letu safari hii wametoza faini ya uharibifu wa mazingira ng’ombe na mbuzi zinazozidi kila mfugo shilingi 20,000,wamekusanya mamilioni ya shilingi,tumewandikiwa risiti ambazo sio halali tunaomba serikali isikilize kilio chetu, anasema mfugaji Machia.
Wafugaji wahamiaji wengine waliopigwa faini ya kuzidi kwa mifugo na kuandikiwa risiti kuwa  ni faini  kwa ajili ya kulisha mifugo kwenye mashamba ni Misa Njigula wa kijiji cha Totowe ambaye alipigwa faini ya shilingi 1,275,000 kwa ajili ya ng’ombe 255,Masale Gidai wa kijiji cha Magamba alipigwa faini ya shilingi 770,000.

Kiongozi wa kikundi cha wafugaji bonde la Songwe Julius Machia
Masele Julius wa kijiji cha Ifuko alipigwa faini ya shilingi 140,000,Mashala Kwilasa wa kijiji cha Galula  alipigwa faini ya shilingi 115,000 na mfugaji John Kasema wa Totowe ametozwa faini ya shilingi milioni nane kwa ng’ombe 400.
“Tanzania ni nchi  inayosifika kuongoza kwa kufuata utawala wa sheria,sisi wafugaji wahamiaji tumechoka kunyanyaswa, kukandamizwa, kukamatwa ovyo,kutozwa faini zisizo za haki kwanini kama sisi ni wahalifu tusipelekwe mahakamani ili haki itendeke’’,anasema mfugaji Machia.
Sisi wafugaji tulio wengi hatujasoma,tunadhulumiwa mifugo yetu kwa miaka kumi sasa,wewe nenda ukaone maisha ya watumishi wa umma wakiwemo watendaji , madiwani pamoja na viongozi ngazi ya wilaya sisi wenye mifugo tunaonekana masikini,watumishi hao wametajirika kutokana na mifugo yetu’’,anadai  Machia.
Asilimia 90 ya wafugaji wahamiaji  katika Bonde la Songwe hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu hali ambayo inawafanya baadhi ya watendaji serikalini kutumia mwanya huo kuwadhulumu kwa kuwapiga faini ambazo sio halali.
Hata hivyo afisa mifugo na kilimo katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya Adamu Mbale amekiri kuwepo kwa baadhi ya watendaji kuhusika na utoaji wa risiti ambazo sio halali“Kuna watendaji wawili kutoka vijiji vya Bonde la Songwe ambao wamechunguzwa na TAKUKURU  baada ya kubainika kufanya udanganyifu kwenye risiti za malipo na kesi zao zipo mahakamani’.
Deus Mashalla mfugaji katika kijiji cha Galula anasema kitendo cha kukamata mifugo ya wafugaji wahamiaji kimekuwa kinafanyika sio kwa kuangalia idadi ya mifugo inayozidi 70  badala yake  hata wakikuta mfugaji mhamiaji katika eneo lake kuna ng’ombe mmoja hukamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi  na kumtoza mfugaji huyo kiasi cha shilingi 20,000.
Hata hivyo Mashalla anabainisha  kuwa wanaoendesha operesheni ya kukamata mifugo wamekuwa wanavamia hata katika nyumba za wafugaji wahamiaji na kuwanyang’anya mifugo na kuwatendea  vitendo  vinavyokwenda kinyume na haki za binadamu.
Anavitaja vitendo hivyo kuwa ni kutishiwa risasi hewani ili wenye mifugo wajifiche na kuogopa kuuwawa,kupiga nyumba risasi hadi kubomoa ambapo wametolewa mfano nyumba ya mfugaji Jikolela Mihambo wa kijiji cha Swela nyumba yake iliteketea kwa moto baada ya kupigwa kwa risasi.

Afisa mifugo na kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Adamu Mbale
Vitendo vingine ambavyo vinakiuka haki za binadamu ni kuporwa kwa fedha za wafugaji,mgambo na askari kuwakimbiza wafugaji kwa magari na kuwasababishia majeraha wakati wakijitahidi kukimbia ili kujiokoa.
Wafugaji wahamiaji hao wamebainisha zaidi kuwa wafugaji wa bonde la Songwe ndiyo jamii inayooongoza kwa kilimo  kwa kuwa wanazalisha mazao mengi ya chakula kama vile mahindi,mpunga,mtama na viazi vitamu na kwamba wafugaji hawapati tatizo la njaa ukilinganisha na wakulima wenyeji ambao karibu kila mwaka wanapata tatizo la njaa.
Gamaya Bunga  mfugaji katika kijiji cha Chang’ombe anasema  utozwaji wa faini unaonekana kufanyika kwa upendeleo kwa kuwa wakulima wanaovunja sheria na kulima kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria kama vile kwenye vyanzo vya maji  vya mto Songwe na ziwa Rukwa hawakamatwi.
Bonde la Songwe lenye kata za Galula, Mbuyuni, Totowe, Namkukwe na Khanga lina utajiri mkubwa wa mifugo inayomilikiwa na wafugaji wahamiaji kutoka wa mikoa ya Tabora ,Shinyanga, Mwanza, Singida na Kagera ambapo inakadiriwa  kuna mifugo zaidi ya 727,230 hadi kufikia mwaka jana.
Takwimu ambazo zimetolewa na afisa mifugo,kilimo na ushirika katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya Adamu Mbale  zinaonesha kuwa  kati ya mifugo hiyo ng’ombe ni 286,800, mbuzi 46,501, kondoo 24,803, nguruwe 11,223 na kuku wa kienyeji 357,903.
Mbale anabainisha kuwa Kutokana na uwepo wa mifugo mingi serikali mwaka 2002 ilitoa sheria ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya  kuhakikisha kila mfugaji katika bonde hilo awe na mifugo isiyozidi 70 na kwamba mfugaji atakayezidisha kiwango hicho cha mifugo anapigwa faini  ya shilingi 20,000 kwa kila mfugo unaozidi.
Operesheni ya kukamata mifugo iliyozidi ilikuwa inafanyika tangu mwaka 2001 hadi 2010 katika Bonde la Songwe kwa kuhusisha wadau mbalimbali wakiwemo watendaji wa serikali, mgambo, na polisi, hata hivyo kuanzia mwaka jana mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro alipiga marufuku operesheni hiyo akitaka wafugaji kwanza wapewe elimu ya kutosha.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro katika kukabiliana na uingizaji wa mifugo ametoa wito kwa   wakuu wa wilaya tisa zinazopakana na wilaya yake wasitishe utoaji wa vibali vya kusafirishia mifugo hasa Ng’ombe wanaoingia wilayani humo.
Wilaya zilizofikia muafaka wa kutotoa vibali vya uingizaji na utoaji wa vibali vya mifugo ni pamoja na Chunya, Mbarali, Mbeya, Mbozi, Mpanda, Sumbawanga, Sikonge, Urambo na Manyoni.